rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Rwanda Uganda Sierra Leone Australia

Imechapishwa • Imehaririwa

Wanariadha kutoka Afrika waendelea kutoweka Australia

media
Serikali ya Australia inawatafuta wanariadha kutoka Afrika wanaoendelea kutoweka nchini humo. REUTERS/David Gray

Waandalizi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola wanasema wanariadha wengine watano kutoka mataifa ya Afrika wametoweka na hawajulikani walipo.


Hii imekuja baada ya wengine nane kutoka Cameroon kutoweka na kwenda kusikojulikana.

Waandalizi wa michezo hiyo wanasema wanariadha hao ni kutoka Rwanda, Uganda na Sierra Leone na wanachunguza ili kufahamu wamekwenda wapi.

Kawaida wakati wa michezo kama hii, wanariadha hupewa muda zaidi wa kuishi katika nchi ambayo mashindano hayo yanafanyika. Mfano mzuri ni mwaka 2000 wakati wa mashindano haya jijini Sydney, wanaridha zaidi ya 100 waliendelea kuishi katika jiji hilo hata baada ya kumalizika kwa michezo hiyo.

Serikali ya Australia imetoa visa kwa wanamichezo wanaoshiriki katika michezo hiyo, kuendelea kuwa nchini humo hadi tarehe 15 mwezi Mei.