rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza Manchester City Liverpool FC Barcelona AS Roma

Imechapishwa • Imehaririwa

Man City kumenyana na Liverpool

media
Sergio Aguero na Leroy Sane (Manchester City), wakati wa mechi ya Manchester City dhidi ya Arsenal, Novemba 5, 2017. REUTERS/Phil Noble

Manchester City wanawakaribisha Jumanne ya wiki hii nyumbani kwao kwenye uwanja wa Etihad klabu ya Liverpool, ambayo imesema imejipanga kufanya vizuri ugenini.


Katika mchezo huu wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya Man City watakuwa na kibarua kizito kwa kuweza kupata ushindi. Man City wanatakiwa kuifunga Liverpool bao 4-0 baada ya mechi iliyopita kufungwa 3-0 kwenye uwanja wa Anfield mjini Liverpool.

Hata hivyo Man City wamesema wanajiamini na watafanya vizuri wakiwa nyumbani na wala hawataangusha mashabiki wao.

Katika mchezo mwingine wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya, AS Roma itashuhudiwa wakimenyana na Barcelona katika uwanja wa Stadio Olimpico.

Meneja wa Roma Eusebio di Francesco amekiri kwamba kwa hakika kukutana na Barcelona anakutana na alichokiita Mashine lakini anabaki na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.