Pata taarifa kuu
MECHI ZA KIRAFIKI

Hispania, Brazil na Ufaransa zapata ushindi mechi za kimataifa za kirafiki

Mataifa ya Ufaransa, Hispania na Brazil yameibuka na ushindi katika mechi za kimataifa za kirafiki zilizochezwa katika miji mbalimbali duniani.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazili na Ujerumani wakati walipocheza mchezo wa kirafiki, Machi 27, 2018.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazili na Ujerumani wakati walipocheza mchezo wa kirafiki, Machi 27, 2018. REUTERS/Wolfgang Rattay
Matangazo ya kibiashara

Mechi hizo zinachezwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kandanda Duniani (Fifa), zilizochezwa jana.

Hispania ambao walikuwa mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2010 wailipata ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Argentina huku mshambuliaji wa Real Madridm Isco akifunga mabao matatu, Ufaransa iliwachapa wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka huu, Urusi kwa mabao 3-1.

Timu nyingine zilizopata ushindi ni Brazil ambayo iliwachapa mabingwa wa Kombe la Dunia, Ujerumani kwa bao 1-0 lililofungwa na Gabriel Jesus. Croatia iliichapa Mexico kwa bao 1-0 na Peru iliichapa Iceland kwa mabao 3-1 nayo Ubelgiji iliishinda Saudi Arabia kwa mabao 4-0.

Wawakilishi wa bara la Afrika katika Kombe la Duniam Misri walishindwa kutamba mbele ya Ugiriki kwa kufungwa kwa bao 1-0 wakati wawakilishi wengine wa Afrika, Tunisia waliishinda Costa Rica kwa bao 1-0.

Matokeo ya mechi nyingine za kirafiki zilizochezwa jana

Italia ilifungana bao 1-1 na England

Bosnia&Herzegovina ilitoka suluhu na Senegal

Denmark pia ilitoka sare ya bila kufungana na Chile

Ivory Coast iliichapa Moldova kwa mabao 2-1

Romania iliifunga Sweden kwa bao 1-0

Iran pia iliifunga Algeria mabao 2-1

Georgia iliifunga Lithuani mabao 4-0

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.