rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Manchester City Pep Guardiola

Imechapishwa • Imehaririwa

Pep Guardiola, awashukuru wamiliki wa Manchester City kwa kumvumilia

media
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola (Kushoto) akisherehekea goli mwezi Februari mwaka 2018 Reuters/Carl Recine

Kocha wa klabu ya soka ya Manchester City Pep Guardiola, amewashukuru wamiliki wa klabu hiyo kutoka Falme za Kiarabu kwa kumvumilia baada ya kushinda ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza alipoanza kuifunza msimu wa mwaka 2016/17.


Guardiola, anaelekea kuiongoza timu yake kunyakua taji la ligi kuu msimu huu kwa sababu inaongoza ligi kwa alama 78, baada ya mechi 29 ikifuatwa na Manchester United ambayo ina alama 65 baada ya mechi 30.

Kuna tofauti ya alama 13 kati ya timu hizi mbili kuelekea kumalizika kwa msimu wa ligi mwezi Mei.

Ushindi dhidi ya Stoke City siku ya Jumatatu, utaihakikishia zaidi Manchester City kunyakua ubingwa msimu huu kwa sababu itakuwa inaongoza alama 18 zaidi.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina Sergio Aguero, atakosa mchuano wa Jumatatu na atasalia nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili baada ya kupata jeraha la goti wakati akiwa mazoezini.

Kocha Guardiola anatarajiwa kukutana na Mwenyekiti wa klabu hiyo Khaldoon al Mubarak baada ya mechi ya Jumatatu.