rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Maandamano nchini Iraq: Takwimu rasmi za watu waliouawa ni 157, pamoja na 111 Baghdad
  • Machafuko Chile: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 15 baada ya watu watatu kuuawa (serikali)
  • Rais wa Chile Piñera ajaribu kutuliza hasira za waandamanaji baada ya maandamano mapya

FIFA Tanzania CAF Gianni Infantino Ahmad Ahmad TFF

Imechapishwa • Imehaririwa

Infantino awasili Tanzania,kuongoza mkutano wa Fifa

media
Rais wa Fifa, Gianni Infantino REUTERS/Rupak De Chowdhuri

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani Gianni Infantino amewasili Tanzania alfajiri ya leo kuhudhuria mkutano wa shirikisho hilo, ameambatana na Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika CAF, Ahmad Ahmad.


Katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Infantino amelakiwa na Waziri wa Haabari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, Rais wa TFF, Wallace Karia na mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Leodgar Tenga.

Mkutano huo wa Fifa unafanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere Mjini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumpokea kiongozi huyo Waziri Mwakyembe amesema Tanzania iko tayari kutoa ushirikiano kwa mikakati mbalimbali ya Fifa yenye lengo la kuinua soka la Afrika.

“Tunawaunga mkono na Tanzania iko tayari kushirikiana na Fifa, tunawatakia mkutano mwema na tunawahakikishia amani na usalama katika muda wote watakaokuwa hapa,”alisema Mwakyembe.

Agenda kadhaa zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa Fedha za FIFA kwaajili ya maendeleo ya mchezo wa soka, changamoto za usajili wa wachezaji kwa kutumia mtandao yaani Transfer Matching System (TMS) na kalenda ya kimataifa ya FIFA.

Baadhi ya nchi zitakazoshiriki katika mkutano huo ni Bahran, Saudi Arabia, Palestina, Algeria,Ivory Coast, Tunisia, Mali na Niger.

Hata hivyo, mkutano huo hautajadili agenda yoyote kuhusu Tanzania na hivi karibuni mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Yusuph Singu alisema serikali ya Tanzania inakusudia kutoa mwaliko rasmi kwa Fifa ili kuja kwa minajili ya kutathimini maendeleo ya soka la Tanzania.

Ripoti ya Mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka