Pata taarifa kuu
CAF-KLABU BINGWA AFRIKA-KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA-SIMBA-YANGA

Yanga, Simba zaenda ugenini kusaka tiketi ya kufuzu hatua inayofuata ya michuano ya klabu Afrika.

Mabingwa wa soka nchini Tanzania, Yanga wamesafiri kuelekea nchini Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya klabu ya St. Louis ya Shelisheli. Yanga imeondoka na wachezaji 20 na viongozi 10 akiwemo kocha George Lwandamina na msaidizi wake Shadrack Nsajigwa.

-
- CAF
Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo huo, Yanga ambao ni mabingwa mara 27 wa soka nchini Tanzania wanahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua inayofuata baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.

Katika mchezo huo, Yanga itawakosa Donald Ngoma, Yohana Mkomola, Amisi Tambwe na Abdallah Shaibu ambao wamekuwa na majeruhi ya muda mrefu. Pia taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema wachezaji Obrey Chirwa na Thaba Kamusoko watakosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismass Ten amesema nia ya timu yake ni kupata matokeo ili kufuzu hatua inayofuata.

Yanga iliondoka nchini Tanzania asubuhi ya leo na kupitia Nairobi nchini Kenya na endapo itashinda mchezo huo itachuana na El- Merreikh ya Sudan au Township Rollers ya Botswana

Katika hatua nyingine, Simba inaondoka nchini leo saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kuelekea nchini Djibout kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Gendermarie Nationale.

Mchezo huo utachezwa February 20 nchini Djibout huku Simba ikijivunia ushindi wa mabao 4-0 iliopata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Simba umetangaza majina ya wachezaji 20 akiwemo mshambuliaji John Bocco ambaye aliumia kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui.

Wachezaji wengine wanaoondoka ni Aishi Manula, Emanuel Mseja, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin, Bukaba Paul Bundala, Emanuel okwi, Moses Kitandu, Shiza Kichuya, Nicholas Gyan, Erasto Nyoni, James Kotei, Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Ally Shomari, Said Ndemla, Yusuph Mlipili, Juuko Murshid na Asante Kwasi.

Kikosi hicho kitaongozwa na Kocha Mkuu, Pierre Lechantre na Kocha msaidizi, Masoud Djuma na viongozi wengine wa klabu hiyo.

Endapo Simba itashinda mchezo huo itakutana na mshindi baina ya Green Buffalo ya Zambia au Al Masry ya Misri.

Ripoti ya mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.