Pata taarifa kuu
ARSENAL-DORTMOND-SOKA-MICHEZO

Aubameyang ahamia Arsenal

Mchezaji nyota kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ameachana na klabu yake ya Dortmund na kuhamia Arsenal, kwa mujibu wa klabu hiyo ya Uingereza.

Pierre-Emerick Aubameyang akikabiliana na Iban Iyanga kutoka Eguatorial Guinea.
Pierre-Emerick Aubameyang akikabiliana na Iban Iyanga kutoka Eguatorial Guinea. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Hakuna mara hata moja katika historia ndefu ya ligi kuu wa Ujerumani Bundesliga ambapo mchezaji kutoka Afrika alikuwa ameongoza kwa ufungaji wa mabao ligini peke yake hadi pale Pierre-Emerick Aubameyang alipofunga mabao 31 msimu wa 2016-17.

Idadi yake ya mabao ilimuwezesha raia huyo wa Gabon kuvunja hata rekodi iliyowekwa na mchezaji wa Ghana Tony Yeboah, ambaye alimaliza akiwa anashikilia nafasi ya ufungaji mabao ligini na mchezaji mwingine miaka ya 1990.

Aubameyang alifunga mabao 141 katika mechi 213 akiichezea Dortmund tangu 2013, ikiwemo mechi 21 kati ya 24 msimu huu.

Hivi karibuni meneja wa Arsenal Arsene Wenger alithibitisha kwamba klabu hiyo inataka kumnunua mchezaji wa Borussia Dortmund mzaliwa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang .

Kufikia sasa msimu huu Aubameyang amefunga mabao 13 katika mechi 15 alizocheza.

Alifunga mabao 31 katika mechi 32 msimu uliopita na kwa sasa amepungukiwa na mabao mawili pekee kufikisha mabao 100 aliyoyafunga tangu atue Ujerumani mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.