rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

FIFA Morocco Afrika Kusini

Imechapishwa • Imehaririwa

Morocco yazindua kampeni ya kutaka kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2026

media
Uzinduzi wa Morocco kutafuta nafasi ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia 2026 soccer-news

Morocco imezindua kampeni ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia katika mchezo wa soka jijini Casablanca mwaka 2026.


Hii ni mara ya tano kwa taifa hilo la Afrika Kaskazini, kuomba wenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani baada ya kujaribu tena 1994, 1998, 2006 na 2010 bila mfanikio.

Nchi hiyo inashindana  na Canada, Mexico na Marekani ambazo zimeomba kuandaa michuano hii kwa pamoja.

Shirikisho la soka duniani FIFA, linatarajiwa kutangaza mwenyeji wa michuano hiyo tarehe 13, siku moja kabla ya kuanza kwa fainali ya mwaka huu nchini Urusi.

Mwenyekiti wa Kamati inayowasilisha maombi hayo Moulay Hafid Elalamy, amesema Morocco inataka kuonesha dunia kuwa, ndio kitovu cha mchezo wa soka.

Hata hivyo, haijafamika Morocco imepanga kutumia viwanja gani katika michuano hiyo.

Afrika Kusini hadi sasa ndio nchi pekee ya Afrika ambayo imewahi kuwa wenyeji wa michuano hii mwaka 2010.

Kwa mara ya kwanza, mataifa 48 yatashiriki katika fainali ya kombe la dunia kutoka timu 32.