rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania Burundi Yanga SC Simba SC

Imechapishwa • Imehaririwa

Golikipa wa zamani wa Simba, Yanga afariki nchini Burundi

media
Golikipa wa zamani wa Simba, Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Ismail Suma enzi za uhai wake facebook/patrick mrope

Golikipa wa zamani wa Simba, Yanga afariki nchini Burundi Kipa wa zamani wa Timu za Simba na Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Ismail Suma amefariki leo akiwa nchini Burundi.


Mbali na kuzichezea Simba na Yanga, kipa huyo pia aliwahi kuichezea Mbagala Markets ambayo baadaye ilibadilishwa na kuitwa African Lyon ambayo aliipandisha daraja mwaka 2009.

Mchezaji wa zamani wa aliyecheza na Suma, Patrick Mrope ameiambia RFI Kiswahili kwamba Suma, amefariki dunia akiwa nchini Burundi alikokwenda kutafuta maisha.

“Alikuwa kipa mzuri lakini hakudumu sana kwenye mpira wa Tanzania kutokana na ubabaishaji, tunawasiliana na wadau mbalimbali wa soka ili kusaidia kurudisha mwili wake Tanzania.

Ripoti na Mwandishi wa RFI Kiswahili