rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Riadha Rio Olimpiki 2016

Imechapishwa • Imehaririwa

Samuel Muchai atajwa mchezaji bora nchini Kenya

media
Washindi wa tuzo ya SOYA mwaka 2018 nchini Kenya www.the-star.co.ke

Mwanariadha wa Kenya Samuel Muchai ametajwa kuwa mwanamichezo bora kwa mwaka 2017, baada ya kupigiwa kura na wanahabari wa michezi nchini humo.


Muchai ambaye ni mwanariadha mlevu, alishinda tuzo hiyo inayofahamika kama SOYA baada ya kushinda medali mbili za dhahabu wakati wa mashindano ya Olimpiki kwa walemavu mwaka 2016 nchini Brazil.

Tuzo ya Wanariadha wa mwaka iliwaendea Hellen Obiri na Conseslus Kipruto.

Wawili hao walishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya riadha ya dunia mwaka uliopita jijini London nchini Uingereza.

Obiri mwenye umri wa miaka 28 alishinda mbio za Mita 5,000 huku Kipruto akiibuka wa kwanza katika mbio za Mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Orodha kamili Washindi:

Mwanamichezo bora wa mwaka

Samuel Muchai (Mwanariadha mlemavu)

Mchezaji bora wa kiume

Conseslus Kipruto (Riadha)

Mchezaji bora wa kike

Hellen Obiri (Riadha)

Mchezaji bora chipukizi kwa upande wa kiume

Aman Gandhi (Cricket)

Mchezaji bora chipukizi kwa upande wa kike

Jackline Wambui (Riadha)

Mchezaji bora anayeishi na ulemavu (Kiume)

Samuel Muchai (Paralympics)

Mchezaji bora anayeishi na ulemavu (Kike)

Beryl Wamira (Deaflympics)

Kocha bora wa mwaka

Jimmy Kamande (Cricket)

Timu bora ya mwaka-Kiume

Timu ya taifa ya Cricket chini ya miaka 19

Timu bora ya mwaka-Wanawake

Kenya Lionesses (Raga)

Shirikisho bora la mwaka

Riadha Kenya

Wachezaji mashuhuri

Allan Thigo(Soka) and Stephen Muchoki (Bondia)