rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

FIFA Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa FIFA

media
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino REUTERS/Rupak De Chowdhuri

Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) limeiteua Tanzania kufanyia mkutano wake mkuu wa kila mwaka utakaoshirikisha mataifa 19 ambayo ni wanachama wa Shirikisho hilo.


Mkutano huo mkubwa wa Kihistoria umepangwa kufanyika Februari 22 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam  na kuongozwa  na rais wa shirikisho hilo, Giani Infantino.

Baadhi ya agenda zinazotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huo utoaji wa fedha za Fifa kwa ajili ya maendeleo ya soka na changamoto za usajili kwa njia ya mtandao ujulikanao kwa kiingereza Transfer Matching System.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Wallace Karia ameipongeza Fifa kwa kuichagua Tanzania kuandaa mkutano huo na kwamba hiyo ni heshima kwa Tanzania.

Ofisa wa mawasiliano kutoka kitengo cha habari, TFF, Clifford Ndimbo amesema wageni watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili Tanzania Februari, 20.

Mataifa yatakayoshiriki mkutano huo ni Tanzania (mwenyeji), Algeria, Mali, Morocco, Burkinafaso, Angola, Niger, Bahrain, Palestina na Saud Arabia. Mengine ni Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Tunisia, Bermuda, Monserrat, St Lucia, Visiwa vya US Virgin, Maldives na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ripoti ya mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka