Pata taarifa kuu
CECAFA-SOKA-MICHEZO

Uganda Cranes kumenyana na Zanzibar Heroes

Nusu fainali ya pili kuwania taji la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, leo mchana katika uwanja wa Moi mjini Kisumu nchini Kenya.

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars walifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuwashinda Intamba Murugamba bao 1-0 katika michuano ya CECAFA inayoendelea.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars walifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuwashinda Intamba Murugamba bao 1-0 katika michuano ya CECAFA inayoendelea. youtube
Matangazo ya kibiashara

Mabingwa watetezi Uganda Cranes watakuwa wanashuka dimbani kumenyana na mabingwa wa mwaka 1995 Zanzibar Heroes.

Mchuano huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na timu zote kuonesha mchezo wa hali ya juu katika hatua ya makundi.

Jana Alhamisi, wenyeji Harambee Stars walifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuwashinda Intamba Murugamba bao 1-0.

Ushindi wa Kenya, ulikuja katika muda wa zaidi baada ya timu zote mbili kutofungana katika muda wa kawaida wa dakika 90.

Fainali itachezwa siku ya Jumapili.

Hayo yakijiri Uganda imekuwa katika harakati ya kumtafuta kocha mkuu wa timu ya taifa baada ya kujiuzulu kwa Milutin Micho, miezi kadhaa iliyopita,

Rais wa zamani wa soka nchini Zambia Kalusha Bwalya amekuwa akiongoza mchakato wa kumpata kocha huyo.

Mamia ya makocha kutoka maeneo mbalimbali duniani, walituma maombi ya kuifunza Uganda Cranes lakini duru zinasema kuwa Luc Eymael ni miongoni mwa makocha wanaopewa naafsi kubwa ya kupata kazi hiyo.

Raia huyu wa Ubelgiji, amewahi kuwa kocha wa AFC Leopards ya Kenya, AS Vita clUB ya DRC, Al Merrikh ya Sudan , na sasa Free State Stars ya Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.