Pata taarifa kuu
SOKA-CAF-KLABU BINGWA

Wydad Casablabca na Al-Ahly kumenyana katika fainali ya mwisho

Fainali ya pili kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, itachezwa siku ya Jumamosi kati ya Wydad Casablabca ya Morocco na Al-Ahly ya Misri.

Fainali ya kwanza ya kuwania ubingwa wa taji la Afrika, Al Ahly dhidi ya Wydad Cassablanca
Fainali ya kwanza ya kuwania ubingwa wa taji la Afrika, Al Ahly dhidi ya Wydad Cassablanca Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Mchuano huu unakuja wiki moja baada ya timu zote mbili kutoka sare ya bao 1-1 mjini Alexandria katika fainali ya kwanza.

Al Ahly ambao wameshinda taji hili mara nane, watakuwa na kibarua kizito baada ya kukubali Wydad Casablanca, kupata bao la ugenini.

Klabu hii ya Misri imeshinda taji hili mwaka 1982, 1987, 2001, 2005, 2006, 2008, 2012, 2013.

Wydad Casablanca nayo ilishinda taji hili mara moja tu mwaka 1992.

Mshindi atapata kombe la kitita cha Dola za Marekani Milioni Mbili na Laki tano.

Timu hizi mbili, zilikutana katika hatua ya makundi na Wydad Casablanca kuongoza kundi hilo kwa alama 12 na Al Ahly kumaliza nafasi ya pili kwa alama 11.

Katika hatua hii, Wydad Casablanca ilishinda mechi nne, huku Al-Ahly ikishinda mechi tatu.

Historia ya timu zote mbili:-

Mwaka 2011

Ahly 3 Wydad 3

Wydad 1 Ahly 1

Mwaka 2016

Ahly 0 Wydad 0

Wydad 0 Ahly 1

Mwaka 2017

Ahly 2 Wydad 0

Wydad 2 Ahly 0

Fainali ya kwanza:-

Ahly 1 Wydad 1

Fainali ya pili Novemba 4 2017:-

Wydad - Ahly

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.