Pata taarifa kuu
SOKA-CECAFA-KENYA

Michuano ya CECAFA kutumiwa kuhimiza amani na mshikamano nchini Kenya

Baraza la soka la Afrika Mashariki na Kati CECAFA, limesema michuano ya mwaka huu baina ya timu za taifa, itatumiwa kuhubiri amani na mshikamo nchini Kenya, wakati huu nchi hiyo inapoendelea kupitia mvutano wa kisiasa.

Nemboya CECAFA
Nemboya CECAFA cecafa
Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo itakayoyakutanisha mataifa 12 nchini Kenya, itafanyika kuanzia tarehe 25 hadi Desemba tarehe 9 mjini Nakuru, Kakamega na Kisumu, miji inayopatikana Magharibi mwa nchi hiyo.

Miji hiyo ni ngome ya siasa za upinzani, eneo ambalo limekuwa na makabiliano makali kati ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga na polisi na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.

“Michezo imetumiwa kama silaha ya kuhubiri amani katika mataifa mbalimbali, na hivyo tunataka kutumia mchezo wa soka kuwaleta watu pamoja baada ya kipindi kigumu cha kisiasa,” amesema Nicholas Musonye Katibu Mkuu wa CECAFA.

Michuano ya CECAFA inarejea tena, baada ya kufanyika mara ya mwisho mwaka 2015 na Uganda kunyakua taji lake la 14, kwa kuishinda Rwanda bao 1-0 katika mchuano wa fainali.

Mataifa yatakayoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na wenyeji Kenya, Burundi, Ethiopia, Somalia, South Sudan, Sudan, Uganda (Mabingwa watetezi), Tanzania na Zanzibar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.