Pata taarifa kuu
RIADHA

Paul Tergat rais mpya wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya

Bingwa wa zamani wa dunia wa mbio za Marathon Paul Tergat, ametajwa  kuwa rais mpya  wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya NOCK.

Rais mpya wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya Paul Tergat
Rais mpya wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya Paul Tergat /twitter.com/moscakenya?lang=en
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja  baada ya mvutano wa miezi kadhaa kuhusu wajumbe wa kushiriki katika Uchaguzi huo uliokuwa umepangwa kuwachagua viongozi wapya.

Tergat alikwenda katika Uchaguzi huo akiwa mgombea pekee na hivyo akatangazwa kuwa rais mpya bila ya kupata ushinda wowote.

Tergat mwenye umri wa miaka 48 amesema atatumia uzoefu wake katika mchezo wa riadha kuboresha usimamizi wa michezo ya Olimpiki nchini humo na kuongoza kwa wazi.

Kazi kubwa inayomsbiri ni kupambana na madai ya ufisadi yaliyowakabili viongozi waliopita, baada ya michezo ya Olimpiki nchini Brazil mwaka 2016.

Mbali na hilo, changamoto ya baadhi ya wanaridha wa Kenya kubainika kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini ni suala lingine ambalo lipo mbele yake.

Tergat anachukua nafasi ya rais wa zamani Kipchoge Keino, aliyeongoza Kamati hiyo kwa muda wa miaka 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.