Pata taarifa kuu
UFARANSA-SOKA

Chipukizi Mbappé aitwa katika kikosi cha Les Blue

Mshambuliaji wa klabu ya Monaco nchini Ufaransa Kylian Sanmi Mbappé anayeripotiwa kuwa huenda akajiunga na klabu ya Paris Saint-Germain, ametajwa katika kikosi cha timu ya Taifa.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa  Kylian Mbappé.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappé. Reuters / Jean-Pierre Amet
Matangazo ya kibiashara

Mbappe mwenye umri wa miaka 18, ametajwa na kocha Didier Deschamps kuikabili Uholanzi na Luxembourg katika mchuano muhimu wa kufuzu kwa kombe la dunia, fainali itakayochezwa mwakani nchini Urusi.

Kocha Deschamps amesema hasumbuliwi na ripoti kuwa huenda Mbappe akaondoka katika klabu yake na kuongeza kuwa, ni mchezaji mwenye bidii na ameendelea na mazoezi kama kawaida.

Hata hivyo, wachezaji Ousmane Dembele anayecheza klabu ya Borrua Dortmund na Benjamin Mendy, anayechezea klabu ya Manchester City, hawajaitwa.

Les Blue inatarajiwa kucheza na Uholanzi Alhamisi ijayo jijini Paris kabla ya kukabiliana na Luxembourg mjini Toulouse tarehe 3 mwezi Septemba.

Kikosi:

Makipa : Alphonse Areola (Paris Saint-Germain), Hugo Lloris (Tottenham/ENG), Steve Mandanda (Marseille)

Mabeki: Lucas Digne (Barcelona/ESP), Christophe Jallet (Nice), Presnel Kimpembe (Paris Saint-Germain), Laurent Koscielny (Arsenal/ENG), Layvin Kurzawa (Paris Saint-Germain), Djibril Sidibe (Monaco), Samuel Umtiti (Barcelona/ESP), Raphael Varane (Real Madrid/ESP)

Viungo wa Kati: N'Golo Kante (Chelsea/ENG), Thomas Lemar (Monaco), Blaise Matuidi (Juventus/ITA), Paul Pogba (Manchester United/ENG), Adrien Rabiot (Paris Saint-Germain), Corentin Tolisso (Bayern Munich/GER)

Washambuliaji: Kingsley Coman (Bayern Munich/GER), Nabil Fekir (Lyon), Olivier Giroud (Arsenal/ENG), Antoine Griezmann (Atletico Madrid/ESP), Alexandre Lacazette (Arsenal/ENG), Kylian Mbappe (Monaco), Florian Thauvin (Marseille)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.