Pata taarifa kuu
CAF-FIFA

CAF ina imani kuwa Morocco itaomba wenyeji wa kombe la dunia 2026

Afisa wa Shirikisho la soka barani Afrika Amaju Pinnick ameliambia Shirika la Habari la Uingereza BBC kuwa, nchi ya Morocco itafanikiwa kuomba nafasi ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2026 kufikia makataa ya mwezi ujao.

Uwanja wa Kimataifa wa soka jijini Doha, Qatar utakaoandaa fainali ya kombe la dunia mwaka 2022
Uwanja wa Kimataifa wa soka jijini Doha, Qatar utakaoandaa fainali ya kombe la dunia mwaka 2022 REUTERS/Ibraheem Al Omari
Matangazo ya kibiashara

Moroco itaungana na mataifa mengine duniani kufikia tarehe 11 kuomba nafasi hiyo adhimu kuwa mwenyeji wa michuano hiyo

Marekani, Canada na Mexico ni mataifa mengine ambayo yameomba nafasi ya kuandaa kombe hilo la dunia.

CAF imesema kuwa itaunga mkono ombi la Morocco kama ilivyofanya kwa Afrika Kusini mwaka 2010.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa taifa hilo la Afrika Kaskazini kuomba kuandaa michuano hii.

Imewahi kufanya hivyo mwaka 1994, 1998, 2006 na 2010 bila mafanikio.

Ikiwa Moroco itafanikiwa, itakuwa mara ya pili kwa taifa la Afrika kuandaa michuano hiyo baada ya Afrika Kusini mwaka 2010.

Urusi itaanda michuano ya mwaka 2018, huku Qatar nayo ikiwa mwenyeji wa michuano ya mwaka 2022.

Kombe la dunia hufanyika kila baada ya miaka minne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.