Pata taarifa kuu
UCHUNGUZI-AFCON

Soka Afrika: Mashabiki wapiga kura AFCON kupigwa kila miaka 2 mwezi Juni

Mashabiki watatu wa soka barani Afrika kati ya wanne wanataka Kombe la mataifa barani Afrika (AFCON) liendelee kupigwa kila miaka 2, wakati ambapo wawili kati ya watatu wanapendelea michuano ya Kombe hilo ichezwe mnamo mwezi Juni badala ya mwezi Januari. Haya ni matokeo ya uchunguzi ulioendeshwa na RFI kwa watu takriban 9,000.

Tuzo wanaokabidhiwa washindi wa AFCON.
Tuzo wanaokabidhiwa washindi wa AFCON. GABRIEL BOUYS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo Shirikisho la Soka barani Afrika linatazamiwa kutoa hatma ya AFCON tarehe 18 na 19 Julai 2017.

Maelezo

"Hapana" kwa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kupigwa kila miaka minne badala ya miwili. "Ndiyo" kwa michuano ya AFCON kuchezwa mnamo mwezi Juni na Julai badala ya Januari na Februari. Kuongeza idadi ya timu katika hatua ya fainali?

Kwa nini, michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika isiwe ikiandaliwa mzunguko, kila nchi ikipewa nafasi ya kuandaa michuano hii ya soka barani Afrika.

Hivi ndivyo unaweza kupata kwa ufupi matokeo ya uchunguzi uliofanywa na RFI kwa watu takriban 9,000 kwa Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, Kiswahili na Kireno. Majibu ambayo, kwa bahati mbaya, hatukuweza kuongeza kwa maelfu yaliyotolewa na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Kwa mshangao mkubwa, washiriki wanaona michuano hii ya AFCON ichezwe mnamo mwezi Juni.

Ikiwa kwenye tovuti zetu, kwenye akaunti zetu za Facebook na Twitter matokeo ni sawa.

Idadi kubwa ya washiriki (74.8%) wanaunga mkono michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kupigwa kila miaka miwili. "AFCON yaangaliwa na wengi Afrika, mashindano makubwa yanayongaliwa na watu wengi barani Afrika na duniani ote, amebaini mmoja wa wapiga kura, katika maoni yake. Micuano hii kuchezwa kila miaka minne, ni kuua mpira wa miguu barani Afrika. "

Kuhusu kipindi ambapo mashindano yanaweza kupigwa, hata hivyo, washiriki wameshangaza wengi, karibu watu wawili kati ya watatu (60.6%) wanapendelea michuano hii ichezwe mwezi Juni na Julai. Shirikisho la Soka barabi Afrika (CAF) linatetea kwa miaka kadhaa michuano hii ichezwe mwezi Januari na Februari. "Kwa mwezi Juni na Julai ni msimu wa mvua katika nchi nyingi za Afrika, ameema mshiriki mmoja. Kuna kuwa hakuan joto, hali ambayo itapelekea wachezaji kuwa vizuri na kuleta matiunda kwatimu zao. "

Timu nyingi, ndiyo. Lakini idadi yenyewe ipi ?

Kwa idadi ya timu katika michuano ya AFCON, maoni mengi yamegawanywa. Kwa wale wanaopendelea timu 16. Kundi hili limekusanya kura nyingi (40.9%). Mashabiki wengi wagependa kuona timu zaidi katika hatua ya fainali. Kwa wale wanaopendelea timu 24. Kundi hili limekusanya (34.6%). Kwa wale wanaopendelea timu 20 wamekusanya (20.6%). Kwa wale wachache (0.6%) wanapendelea nchi 32 zishiriki katika michuano ya Kombe la AFCON.

Hatimaye watumiaji wa internet wametoa maoni yao kuhusu timu zinazotakiwa kuandaa michuano hii. Wale wanaopendelea michuano hii kuandaliwa mbali kidogo na bara la Afrika ni 73%.

CAF ndio yenye uamuzi

Shirikisho la Soka Afrika, ambalo linatafakari hatma ya michuano ya AFCON tarehe 18 na 19 Julai nchini Morocco, wanaelewa matokeo haya yote. kongamano hili, lililopendekezwa na rais CAF Ahmad litaruhusu "kuandika ukurasa wa historia katika mabadiliko ya soka barani Afrika. "

"Timu ya sasa inayoonoza Shirikisho la Soka Afrika halipaswi kutufanya kuamini kuwa linahudumu katika Shirikisho la kimataifa la Soka, hata hivyo, ameonya mmoja wa washiriki. Kwa uhakika

Waafrika walihitaji mabadilikokatika uongozi wa taasisi hii. Lakini si kuharibu taasisi hii ".

Michuano ya AFCON inaweza kuchezwa kila miaka minne? *

Ndiyo: 24%

Hapana, kila baada ya miaka miwili: 74.8%

Hakuna maoni: 1,2%

AFCON inaweza kuchezwa mnamo mwezi Juni na Julai? *

Ndiyo. 60.6%

Hapana, ichezwe mnamo mwezi Januari na Februari: 36.4%

Hakuna maoni: 3%

Ni idadi ipi bora ya timu zinazotakiwa kucheza katika hatua ya fainali? *

16, kama ilivyo: 40.9%

20: 20.6%

24: 34.6%

Hakuna maoni: 2.5%

Nyingine: 1.6%

AFCON inaweza kuchezwa mbali na Afrika kila toleo?

Ndiyo, inabidi kuepo na mzunguko: 73%

Hapana: 22.3%

Hakuna maoni: 3.9%

Nyingine: 0.8%

Kumbuka: uchunguzi huu uliendeshwa na RFI kuanzia Juni 23 hadi Julai 17.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.