Pata taarifa kuu
SOKA-COSAFA

Michuano ya COSAFA kuanza siku ya Jumapili

Makala ya mwaka 2017 kuwania ubingwa wa soka kwa mataifa ya Kusini mwa bara la Afrika COSAFA, itafungua milango yake nchini Afrika Kusini kuanzia siku ya Jumapili na tarehe 25 Mwezi Juni mwaka huu.

Ratiba ya michuano ya COSAFA 2017
Ratiba ya michuano ya COSAFA 2017 tff
Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo itapigwa katka viwanja viwili ule wa Moruleng na Royal Bafokeng mjini Rustenburg.

Mataifa 14 yanayoshiriki katika michuano hii ni pamoja na wenyeji Afrika Kusini, Angola, Botswana, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Ushelisheli na Swaziland.

Mataifa mengine ni pamoja na Tanzania ambayo imealikwa lakini pia Zambia na Zimbabwe.

Ratiba ya michuano hiyo:-

Kundi la A

Juni tarehe 25 2017

Tanzania vs Malawi

Mauritania vs Angola

Kundi B

Juni 26 Jumapili 2017

Msumbiji vs Zimbabwe

Madagascar vs Ushelisheli

Mshindi wa kundi A atamenyana na Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali huku, mshindi wa kundi B akicheza na Swaziland. Mechi hizo zitachezwa tarehe 2 mwezi Julai.

Bostwana itacheza na Zambia katika hatua ya robo fainali, huku Namibia wakimenyana Lesotho, mechi zitakazochezwa tarehe 1 mwezi Julai.

Fainali itachezwa tarehe 7 mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.