Pata taarifa kuu
SOKA

Wakala wa Tiote ataka wanahabari kuacha kuuliza mazingira ya kifo cha mchezaji huyo

Wakala wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na klabu ya Beijing Enterprises nchini China, Cheick Tiote aliyefariki dunia wiki iliyopita akiwa mazoezini, amewataka wana habari kuacha kujadili na kukisia kilichosababisha kifo cha mchezaji huyo.

Picha ya Cheick Ismael Tiote akiwa hai
Picha ya Cheick Ismael Tiote akiwa hai REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Emanuele Palladino ametoa wito na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kuihurumia na kuomboleza na familia ya Tiote na kuacha kujiuliza maswali yasiyo na majibu.

Kifo cha mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle nchini Uingereza, alikocheza kwa muda wa miaka saba, kiliwashtua watu wengi na kuleta huzini kubwa kwa wapenzi wa soka duniani.

Mchezaji huyo aliagwa siku ya Jumanne huku mwili wake ukitarajiwa kurejeshwa nyumbani siku ya Alhamisi kwa taratbu zingine za mazishi.

Cheick Tiote aliichezea nchi yake mara 52 na kuisaidia kunyakua taji la bara Afrika 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.