Pata taarifa kuu
UEFA-REAL MADRID-ATLETICO MADRID-SOKA

UEFA: Real Madrid yaichapa Atletico Madrid

Real Madrid kupitia kiungo wake Christiano Ronaldo imeburuza Atletico Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa siku ya jumanne katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu jijini Madrid, nchini Uhispania.

Wachezaji wa timu ya Real Madrid wakishangilia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Atletico Madrid. .
Wachezaji wa timu ya Real Madrid wakishangilia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Atletico Madrid. . REUTERS/Heino Kalis
Matangazo ya kibiashara

Mabao yote matatu ya Reala Madrid yamepachikwa na Christiano Ronaldo na hivyo kuipelekea klabu yake kupiga hatua katika nusu fainali ya kwanza.

Ronaldo aliweka wavuni bao lake la kwanza katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza na kuandika bao la pili dakika ya 73 kipindi cha pili, huku bao la tatu alikilifunga katika dakika ya 86 kipindi cha pili.

Mechi nyingine itakayopigwa leo Jumatano usiku katika hatua ya nusu fainali ni kati ya FC Monaco dhidi ya Juventus katika uwanja wa Louis jijini Monaco.

Itafahamika kwamba kiungo wa Fc Monaco Radamel Falcao amesema hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo.

FC Monaco inafukuzia mataji mawili msimu huu, taji la la Ligue 1 na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hayo yakijiri Manchester United ambayo inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa nusu fainali ya ligi kuu ya Ulaya siku ya Alhamisi, inaweza kuwakosa nyota wake saba wa kikosi cha kwanza.

Wachezaji hao ambao wanaweza kukosekana katika mchezo huo ni pamoja na Bailly au Chris Smalling pamoja na Phil Jones ,wengine ni Zlatan Ibrahimovic, marcos Rojo na Tomothy Fosu-Mensah.

Hata hivyo Paul Pogba anatarajiwa kurejea katika mchezo huo utakaofanyika nchini Uhispania baada ya kukosa mechi mbili kutokana na kuwa na majeruhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.