Pata taarifa kuu
RIADHA

Keitany avunja rekodi ya dunia katika mbio za Marathon za London kwa wanawake

Mwanariadha kutoka Kenya  Mary Keitany amevunja rekodi ya dunia katika mbio za Marathon kwa upande wa wanawake baada ya kushinda mbio za mwaka huu za London Marathon nchini Uingereza kwa muda wa saa 2, dakika 17 na sekunde 1.

Mkenya Mary Keitany alivyoshinda mbio za London Marathon Aprili 23 2017
Mkenya Mary Keitany alivyoshinda mbio za London Marathon Aprili 23 2017 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Keitany, mwenye umri wa miaka 35, amevunja rekodi iliyowekwa na Paula Radcliffe raia wa Uingereza mwaka 2005 baada ya kukimbia kwa muda wa saa 2 dakika 15 na sekunde 25.

Baada ya ushindi huo, mwanariadha huyo amesema, amefurahi sana kushinda mbio hizi na kuvunja rekodi ya dunia.

Mbali na London  Marathon, Keitany alishinda New York Marathon nchini Marekani mara tatu mfululizo mwaka 2014, 2015 na 2016.

Nafas ya pili ilimwendea Tirunesh Dibaba kutoka Ethiopia,  aliyemaliza kwa muda wa saa 2 dakika 17 na sekunde 56 huku Aselefech Mergia pia kutoka Ethiopia akimaliza wa tatu kwa muda wa saa 2 sekunde 23 :08.

Kwa upande wa wanaume, Mkenya Daniel Wanjiru mwenye umri 24, ameibuka mshindi kwa muda wa saa 2 dakika 5 na sekunde 56.

Wanjiru alimshinda Kenenisa Bekele aliyeonekana kushinda mbio hizi baada ya kumpita katika hatia ya mwishomwisho za mashindano hayo.

Pamoja na ushindi huu Wanjiru amesema bado ana nia ya kuvunja rekodi ya dunia iliyowekwa na Mkenya mwenzake Dennis Kimetto mwaka 2014 jijini Berlin ya saa 2 dakika 02 na sekunde 57.

Mkenya mwingine Bedan Karoki, ambaye ameshiriki kwa mara ya kwanza katika mbio za Marathon  alimaiza wa tatu kwa muda wa saa 2 dakika 07 na sekunde 41.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.