Pata taarifa kuu
RIADHA-KENYA

Sumgong apatikana na kosa la kutumia dawa iliyopigwa marufuku na IAAF

Jemima Sumgong, mwanariadha wa Kenya wa mbio ndefu aliyeshinda medali ya dhahabu katika mbio za Marathon kwa upande wa wanawake wakati wa Michezo ya Olimpiki mwaka 2016 nchini Brazil amebainika kuwa alitumia dawa ya kumwongezea nguvu mwilini.

Jemima Sumgong, mwanariadha wa Kenya alivyoshinda mbio za Marathon wakati wa michezo ya Olimpiki nchini Brazil mwaka 2016
Jemima Sumgong, mwanariadha wa Kenya alivyoshinda mbio za Marathon wakati wa michezo ya Olimpiki nchini Brazil mwaka 2016
Matangazo ya kibiashara

Jemima mwenye umri wa miaka 32 na bingwa wa mbio za London Marathon, amebainika kuwa alitumia dawa iliyopigwa marufuku baada uchunguzi uliofanywa na Shirikisho la mchezo wa riadha duniani IAAF.

Hili ni pigo kwa mwanariadha huyu ambaye hivi karibuni alikuwa ametangaza kuwa atakwenda jijini London tarehe 23 mwezi Aprili kutetea taji lake la London Marathon aliloshinda mwaka uliopita.

Hata hivyo, kumekuwa na uhaba wa maelezo kuhusu uchunguzi huu uliofanywa na IAAF licha ya ripoti za awali kuonesha kuwa mwanariadha huyo alikuwa safi na hakuwahi kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Sumgong alikuwa mwanamke wa kwanza kuishindia Kenya medali ya dhahabu katika mbio za Marathon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.