Pata taarifa kuu
GHANA-SOKA

Kwesi Appiah ateuliwa tena kuwa kocha wa Black Stars

Shirikisho la soka nchini Ghana limemteau tena Kwesi Appiah kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Black Stars.

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah
Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Appiah apewa mkataba wa miaka miwili utakaodumu kuanzia tarehe 1 mwezi Mei.

Anachukua nafasi ya Avram Grant raia wa Israel aliyejiuzulu baada ya kumalizika kwa fainali ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Gabon mwezi Februari.

Itakuwa mara ya pili kwa Appiah kuifunza Black Stars, mara ya kwanza ilikuwa ni kati ya mwaka 2012 hadi 2014.

Mwaka 2014, aliiongoza Ghana katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Kocha huyu atakuwa anajaribu tena kuingoza Ghana kufuzu katika kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi lakini pia   michuano ya Afrika ya CHAN pia mwaka ujao nchini Kenya.

Anarejea katika timu ya taifa akitokea katika klabu ya Al Khartoum nchini Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.