Pata taarifa kuu
AFCON 2017 U 20-ZAMBIA-GUINEA

AFCON 2017 U20: Zambia yaiburuza Guinea

Zambia, wenyeji wa michuano ya AFCON 2017 U20, wamewamenya Guinea bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo katika uwanja wa National Heroes mjini Lusaka.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), linaloongozwa na Issa Hayatou (pichani), laandaa AFCON 2017 U20.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), linaloongozwa na Issa Hayatou (pichani), laandaa AFCON 2017 U20. RFI/David Kalfa
Matangazo ya kibiashara

Timu ya Zambia ilipata bao hilo kupitia mchezaji wake Patson Daka katika dakika ya 48 ya kipindi cha pili cha mhezo katika Kundi B.

Kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Zambia wasiozidi miaka 20 (U20), Beston Chambeshi amekamilisha ndoto yake ya kushinda mechi yake ya kwanza.

"Tunajua kuwa itakuwa vigumu. Ni ushindani mkubwa, pamoja na timu zenye ushindani mkubwa. Ni mashindano makubwa pamoja na timu mashuhuri. Na hiyo ndiyo sababu, kabla ya kuzungumza kuhusu kufika hadi hatua ya mwisho yaani fainali, lazima kufanikiwa kuingia ", alisema Chambeshi kabla ya mchezo.

Mechi ya Kundi B imeendelea siku ya Jumapili, katika mcunao kati ya Misri na Mali.

Kundi A litacheza mechi yake ya kwanza Jumatatu Februari 27, mchuano ambao utazikutanisha timu za Senegal na Sudan saa tisa 9:00 (alaasiri), huku Cameroon na Afrika Kusini wakijitupa uwanjani 12:00 (jioni) saa za kimataifa.

Timu zitakazocheza nusu fainali ya AFCON 2017 U20 zitawakilisha Afrika katika michuano ya Kombe la Dunia kwa timu za taifa za vijana wasiozidi miaka 20 iliyopangwa kuchezwa mwezi Mei na Juni 2017 nchini Korea ya Kusini.

Michuano hii ya AFCON 2017 U20 itamalizika Machi 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.