Pata taarifa kuu
AFCON 2017-GABON-MISRI

Essam El-Hadary ashiriki Afcon 2017 akiwa na umri wa mikaa 44

Kipa wa timu ya taifa ya soka ya Misri, Essam El-Hadary ameweka historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza kushiriki katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika akiwa na umri mkubwa wa miaka 44.

Kipa wa Misri Essam El Hadary, na mchezaji Mohamed Zidan wakifurahi baada ya ushindi wao dhidi ya Ghana.
Kipa wa Misri Essam El Hadary, na mchezaji Mohamed Zidan wakifurahi baada ya ushindi wao dhidi ya Ghana. Reuters
Matangazo ya kibiashara

El-Hadary aliweka rekodi hiyo baada ya kuingia uwanjani wakati wa mchuano dhidi ya Mali siku ya Jumanne usiku uliomalizika sare ya bao 0-0.

Mkongwe huyo aliingia uwanjani baada ya kipa wa kwanza wa Ahmed El-Shenawy kupata jeraha na kulazimika kuingia uwanjani.

Wapenzi wa soka wamempongeza sana El-Hadary kwa hatua hii, pongezi ambazo pia amezipata kutoka kwa Shirikisho la soka duniani FIFA.

Hii imekuwa mechi yake ya 148 kuichezea timu ya taifa tangu mwaka 1996.

El-Hadary alishinda taji hili la Afrika mara ya nne mwaka 1998, 2006, 2008 na 2010.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.