Pata taarifa kuu
TENESI-SERENA

Serena Williams arejea kwa kishindo baada ya kuwa nje kwa miezi 4

Mchezaji anashika nafasi ya pili kwa ubora wa mchezo wa tenesi duniani, Serena Williams, amerejea kwa kishindo baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne, ambapo amepata ushindi katika mzunguko wa kwanza wa mashindano ya ASB Classic mjini Auckland.

Mchezaji tenesi, Serena Williams. Picha ya kumbukumbu 2016
Mchezaji tenesi, Serena Williams. Picha ya kumbukumbu 2016 REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Serena mwenye umri wa miaka 35, ambaye juma lililopita alitangaza kuchumbiwa, alimshinda Mfaransa Pauline Parmentier kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-3 na 6-4.

Williams amekuwa nje ya uwanja akikabiliwa na jeraha la bega na matatizo ya goti toka ilipomalizika michuano ya US Open katika hatua ya nusu fainali mwezi September mwaka jana.

"Mara zote huwa unajisikia vibaya kwenye mechi yako ya kwanza," alisema. " Lakini kiakili nilijua namna nnavyoweza kurejea mchezoni na kufikia kiwango hiki."

Serena ilibidi asubiri kwa siku moja zaidi ili acheze mchezo wake wa kwanza katika mwaka 2017, baada ya siku ya Jumatatu mvua kubwa kunyesha na kusababisha mchezo huo kuahirishwa.

Ilimchukua dakika 74 kumfunga mchezaji anayeshika nafasi ya 69 kwenye orodha ya wachezaji wa mchezo huo, akipiga Aces 8, ikiwemo mchezo mmoja ulioamuliwa kwa alama.

Kwa matokeo haya, Serena sasa atacheza na Mmarekani mwenzake Madison Brengle, anayeshika nafasi ya 74.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.