Pata taarifa kuu
WADA-OLIMPIKI

Mkuu wa shirika la WADA awaomba radhi wajumbe wa kamati ya Olimpiki walioko Qatar

Mkuu wa shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni, WADA, Craig Reedie, ameomba radhi kwa maofisa wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki ambao wamechukizwa na muda ambao shirika hilo limetangaza kuifunga maabara pekee ya kufanya vipimo hivyo nchini Qatar. 

Ofisi za shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni, WADA
Ofisi za shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni, WADA REUTERS/Christinne Muschi
Matangazo ya kibiashara

WADA ilitangaza Jumatatu ya wiki hii kuwa, maabara ya Qatar itasimamisha shughuli zake kwa angalau miezi minne, tangazo linalokuja wakati huu maofisa zaidi ya elfu 1 wa kamati ya Olimpiki wakiwa wamewasili jijini Doha kwa mkutano mkuu wa mwaka wa vyama vya kamati ya Olimpiki.

Maofisa wa kamati ya Olimpiki wanasema kuwa, muda uliotumiwa na WADA kutangaza hatua hiyo, ulilenga kutia doa mkutano wa simu mbili unaoanza mjini Doha, Qatar, mkutano ambao utashuhudia miji ya Budapest, Los Angeles na Paris ikiwasilisha maombi ya kuandaa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2024.

"Naomba radhi kabisa kwa kilichotokea, nisema kuwa hatukufanya hivi kwa makusudi, naahidi," alisema Reedie, mkuu wa shirika la WADA.

"Niliamua kuwa zoezi liwe limehitimika Jumatano ya wiki iliyopita, lakini na imani kuwa kazi kwenye maabara hiyo zitakamilika kabla ya mkutano mkuu mjini Doha". alisema.

Reedie ameongeza kuwa "hakuna wakati mzuri muda wote kutangaza kusimamishwa au hata kuwekwa sheria kali zaidi kwa maabara."

Reedie alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kubanwa na wajumbe kutoka Sudan na Uhispania pamoja na Sheikh Ahmad al-Fahad al-Sabah, rais wa baraza la Olimpiki kwa nchi za Asia na mjumbe wa kamati ya kimataifa ya olimpiki, saa chache baada ya kutoa hotuba yake.

Sabah alionesha kuguswa na uamuzi wa WADA ambapo alidai kuwa ulilenga kutia dosari mkutano mkuu wa kamati ya Olimpiki pamoja na kuidhalilisha nchi ya Qatar.

Sabah ameongeza kuwa hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa maofisa wa kamati ya Olimpiki kudhalilishwa kiasi hiki na shirika la WAD, akitolea mfano muda wa tangazo lenyewe kutoka na ripoti kadhaa pia zilizowahi kutolewa na shirika hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.