Pata taarifa kuu
SOKA-UEFA

Arsenal kuwakosa Coquelin na Giroud katika mchuano dhidi ya Basel FC

Michuano ya soka hatua ya makundi kuwania taji la UEFA, inaendelea Jumatano usiku katika viwanja mbalimbali.

Mchuano uliopita wa Arsenal dhidi ya Basel FC ya Uswizi
Mchuano uliopita wa Arsenal dhidi ya Basel FC ya Uswizi uefa
Matangazo ya kibiashara

Arsenal ya Uingereza itakuwa nyumbani kupambana na Basel FC ya Uswizi katika mchuano wa kundi A.

Kikosi cha Arsenal kitamkosa mchezaji wake wa kutegemewa Francis Coquelin anayeuguza jeraha la goti.

Olivier Giroud ambaye alipewa kadi nyekundu wakati wa mchuano wa kwanza wa kundi hili dhidi ya Paris St-Germain katika mchuano ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 atakosa mchuano huo muhimu.

Arsenal wanakwenda katika mechi hii baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kuishinda Chelsea mabao 3-0 katika mchuano wa ligi kuu nchini Uingereza.

Vikosi vitakavyoingia uwanjani:-

Arsenal: Ospina; Bellerín, Koscielny, Mustafi, Monreal; Xhaka, Cazorla; Walcott, Özil, Iwobi; Alexis Sánchez.

Basel: Vaclík; Lang, Suchý, Balanta, Traoré; Xhaka, Zuffi; Bjarnason, Delgado, Steffen; Šporar.

Ratiba ya mechi zingine za leo:-

  • Celtic vs Manchester City
  • Napoli vs Benfica
  • Borrusia Mönchengladbach vs Barcelona
  • Atletico Madrid vs Bayern Munich

Matokeo ya Jumanne Septemba 27 2016:-

  • Monaco 1-1 Bayer Leverkusen
  • CSKA Moscow 0-1 Tottenham Hotspurs
  • Borrussia Dortmund 2-2 Real Madrid
  • Leicester City 1-0 Porto
  • Sevilla 1-0 Olympique Lyonn
  • Sporting CP 2-0 Legia Warszawa
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.