Pata taarifa kuu
EFL

City na United kukutana tena kwenye hatua ya nne kombe la ligi Uingereza, EFL

Klabu za Manchester United na Manchester City zitakutana kwa mara nyingine kwenye dimba la Old Trafford, katika mzunguko wa nne wa kombe la Ligi, EFL, baada ya juma hili timu hizo kufuzu.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho (kushoto) akiwa na mwenzake wa Manchester City, Pep Guardiola (kulia), wakikumbatiana wakati timu zao zilipokutana hivi karibuni.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho (kushoto) akiwa na mwenzake wa Manchester City, Pep Guardiola (kulia), wakikumbatiana wakati timu zao zilipokutana hivi karibuni. Reuters / Carl Recine Livepic
Matangazo ya kibiashara

Manchester United waliwatupa nje ya michuano hiyo klabu ya Northampton kwa jumla ya mabao 3-1, huku Manchester City wenyewe wakiwatupa nje klabu ya Swansea kwa jumla ya mabao 2-1, na kufanya timu hizo zikutane kwa mara ya pili ndani ya msimu huu, baada ya ushindi wa City, September 10.

Katika mechi nyingine, klabu ya West Ham yenyewe itacheza na wapinzani wake wa jiji la London klabu ya Chelsea, wakati Tottenham wenyewe watasafiri kuwafuata vijogoo vya jiji Liverpool.

Mechi hizi zote zitachezwa kuanzia mwanzoni mwa wiki ya mwezi October, kati ya October 24 na kuendelea.

Manchester City ambayo ilishinda taji hili msimu uliopita kwa kuifunga Liverpool kwenye mchezo wa fainali kwa njia ya matuta, bado haijapoteza mchezo hata mmoja toka kocha Pep Guardiola achukue mikoba kuifundisha timu hiyo.

Kocha Jose Mourinho na timu yake walimaliza mwiko wa kufungwa mechi tatu mfululizo dhidi ya timu ya Northampton, baada ya kushuhudia ikipoteza dhidi ya City, Feyenoord na Watford.

West Ham yenyewe ilipata ushindi wa dakika za lala salama, shukrani kwa mpira wa adhabu uliopigwa na mchezaji wake Dimitri Payet na kuiwezesha timu yake kuchomoza na ushindi dhidi ya Accrington Stanley.

Katika hatua hii ya robo fainali angalau kutakuwa na timu mbili zinazotoka daraja la chini baada ya vijana wa Rafa Benitez klabu ya Newcastle ikipangiwa kucheza na Preston huku Norwoch wenyewe wakisafiri kucheza na Leeds.

Hull City wenyewe watacheza na Bristol City wakati Southampton wao watacheza na Sunderland kwenye mechi nyingine ambayo itazikutanisha timu zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Arsenal wenyewe watacheza na Reading, timu ambayo iliifunga jumla ya mabao 7-5 walipokutana kwenye hatua ya nne ya kombe la ligi mwaka 2012.

Ratiba kamili ni: West Ham v Chelsea, Manchester United v Manchester City, Arsenal v Reading, Liverpool v Tottenham, Bristol City v Hull, Leeds v Norwich, Newcastle v Preston, Southampton v Sunderland.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.