Pata taarifa kuu
EFL-UINGEREZA

Chelsea, Liverpool zatinga hatua ya 4 kombe la Ligi, Leicester City yatupwa nje

Mechi za kuwania kombe la Ligi nchini Uingereza zimeendelea juma hili, huku mabingwa kombe la ligi kuu, Leicester City wakitupwa nje ya kombe la Ligi katika muda wa nyongeza na klabu ya Chelsea.

Mchezaji wa klabu ya chelsea ya Uingereza, Cesc Fabregas, akishangilia moja ya bao aliloifungia timu yake na kuivusha kwenye hatua ya 4 ya kombe la ligi, EFL, 20 September 2016.
Mchezaji wa klabu ya chelsea ya Uingereza, Cesc Fabregas, akishangilia moja ya bao aliloifungia timu yake na kuivusha kwenye hatua ya 4 ya kombe la ligi, EFL, 20 September 2016. Reuters / Darren Staples Livepic
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa kukata na shoka, ulishuhudiwa mchezaji wa Leicester City, Mjapan, Shinji Okazaki akianza kuipatia timu yake mabao mawili ya kuongoza, na kuonekana dhahiri kuwa jahazi la Chelsea litazama.

Lakini dakika chache kabla ya kwenda mapumziko, beki wa kati wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Gary Cahil aliisawazishia timu yake bao na kufanya matokeo yao hadi mapumziko, Leicester kuongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo haikuchukua muda kwa klabu ya chelsea kusawazisha bao kupitia kwa Cesar Azpilicueta.

Mchezo huo ambao ulilazimika kwenda kwenye muda wa nyongeza, ulishuhudia Chelsea ikitumia uzoefu wake kwenye mashindano makubwa, ambapo mchezaji wake Cesc Fabregas aliifungia mabao mawili na kuifanya klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 na kutonga hatua ya nne ya kombe la Ligi, EFL.

Kwenye mechi nyingine, klabu ya Nottingham Forest ilikuwa nyumbani kuwakaribisha washika bunduki wa London, Arsenal, kwenye mchezo ambao Arsenal waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Leeds Unites wao walichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers, huku AFC Bournemuth wakilala katika muda wa nyongeza dhidi ya klabu ya Preston North End kwa mabao 3-2.

Everton wakiwa nyumbani walijikuta wakitupwa nje ya michuanio ya mwaka huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Norwich City, huku Derby County wenyewe wakikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa vijogoo vya jiji Liverpool.

Brighton wakiwa nyumbani walifungwa na klabu ya Reading kwa mabao 2-1, huku Newcastle United wao wakichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolverhampton.

Mechi nyingine zitapigwa siku ya Jumatani ambapo: QPR vs Sunderland, Westham vs Accrington Stanley, Southampton vs Crystal Palace, Swansea City vs Manchester City, Fulham vs Bristol City, Northampton Town vs Manchester United, Tottenham vs Gillingham na Stoke City vs Hull City.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.