Pata taarifa kuu
SOKA

Guardiola ataka msamaha kutoka kwa Yaya Toure, atangaza kuachana na soka la kimataifa

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza, Pep Guardiola, amesema kuwa hatamchagua mchezaji wake Yaya Toure kwenye kikosi chake, hadi pale wakala wake pamoja na yeye mwenyewe watakapomuomba radhi pamoja na wachezaji wenzake.

Kiungo wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure akiwa mazoezini na timu yake, ametakiwa kumuomba radhi kocha wake, Pep Guardiola.
Kiungo wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure akiwa mazoezini na timu yake, ametakiwa kumuomba radhi kocha wake, Pep Guardiola. Reuters / Carl Recine Livepic
Matangazo ya kibiashara

Toure mwenye umri wa miaka 33 hivi sasa, ameichezea klabu yake mchezo mmoja tu toka msimu huu umeanza ambapo pia hakujumuishwa kwenye kikosi cha Man City ambacho kinashiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya, UEFA.

Wakala wake, Dimitri Seluk, hivi karibuni alidai kuwa mchezaji wake alidhalilishwa na kocha Pep Guardiola anapaswa kumuomba radhi ikiwa City haitashinda taji lolote msimu huu.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari juma hili, kocha Guardiola amesema kuwa “ni lazima aniombe radhi, ama sivyo sitamchagua kwenye timu yangu na hatacheza,” alisema kocha huyo.

Mbali na kutaka kuombwa msamaha kutoka kwa mchezaji wake, Guardiola pian anataka msamaha kutoka kwa wakala wake, Seluk ambaye anadai alimkashifu.

Guardiola ameongeza kuwa ulikuwa ni uamuzi mgumu sana kwake kuamua kumuacha nje ya kikosi chake, kiungo huyo.

“Kama alikuwa na tatizo, alipaswa kuzungumza na watu wa klabu,” alisema Guardiola ambaye wakati akiwa kocha wa FC Barcelona alimuuza mchezaji huyo kwa Manchester City.

Kocha huyo amesema kuwa licha ya Toure mwenyewe kurejea kwenye mazoezi mwanzoni mwa juma, bado hajamuita kumuomba radhi.

Guardiola alikuwa akizungumza saa chache baada ya Toure kutangaza kuachana na soka la kimataifa.

Akiichezea timu yake kwa mara ya kwanza mwaka 2004, Toure ameichezea timu yake mara 113 kwenye michezo ya kimataifa, akishinda taji la ubingwa wa Afrika mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.