Pata taarifa kuu
SOKA-CAF

Michuano ya mwisho kufuzu fainali ya vijana wasiozidi miaka 17 barani Afrika kupigwa

Michuano ya soka, mzunguko wa mwisho kufuzu fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wasiodizi miaka 17 mwaka ujao nchini Madadscar zinachezwa mwishoni mwa wiki hii katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF Cafonline
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kumalizika kwa mzunguko wa pili wa michuano hii mwezi Agosti, ambapo vlabu 14 vilimenyana kufuzu katika hatua hii ya mwisho.

Mechi hizi zitachezwa nyumbani na ugenini na washindi saba wataungana na wenyeji Madagascar katika fainali itakayopigwa mwezi Aprili mwaka ujao.

Ratiba ya michuano ya mwishoni mwa wiki:-

  • Ghana vs Ivory Coast
  • Niger vs Gabon
  • Mali vs Ethiopia
  • Senegal vs Guinea
  • Sudan vs Cameroon
  • Tanzania vs Congo
  • Angola vs Comoros

Michuano hii itachezwa nyumbani na ugenini.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.