Pata taarifa kuu
EUROQF UNDER 21

Rashford aifungia timu yake mabao matatu akiichezea kwa mara ya kwanza

Kinda wa klabu wa Manchester United, Marcus Rashford, amefunga mabao matatu wakati akiichezea kwa mara ya kwanza timu yake ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, wakati walipoifunga Norway kwa magoli 6-1 kwenye mchezo wa kufuzu kombe la mataifa Ulaya kwa vijana chini ya miaka 21.

Marcus Rashford, mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uingereza
Marcus Rashford, mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uingereza Reuters / Ed Sykes Livepic
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyu kinda, tayari alishaifungia timu yake bao wakati alipoichezea kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa Ligi kuu na Europa League sambamba ile timu ya taifa ya wakubwa na sasa hii ya vijana walio na umri wa chini ya miaka 21.

Rashford mwenye umri wa miaka 18 hivi sasa, aliifungia timu yake bao katika dakika ya 18 ya mchezo, akipiga shuti akiwa nje ya eneo la 18, kabla ya kuongeza bao akitumia mpira uliokufa na kisha kutamatisha kwa kuifungia bao la tatu timu yake kwa mkwaju wa Penalty.

Wachezaji wengine waliofingia timu yao ni pamoja na Nathaniel Chalobah, Ruben Loftus-Cheek na Lewis Baker.

Ushindi huu unamaanisha kuwa, kikosi cha kocha Gareth Southgate sasa kipo mbele kwa alama mbili dhidi ya Uswisi na kuongoza kundi lake, huku zikisalia mechi mbili tu.
Norway inasilia kwenye nafasi ya tatu kwenye kundi lake.

Timu zote zinazoongoza kundi, zinajihakikishia nafasi ya kucheza michuano hiyo mwakani nchini Poland huku timu inayomaliza kwenye nafasi ya pili katika kila kundi ikitakiwa kucheza mchezo wa ziada kufuzu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.