Pata taarifa kuu
AFCON2017-DRC

AFCON2017: DRC yafuzu kwa hatua ya fainali

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuepo nchini Gabon Januari 2017. Chui wa DRC wamejikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayochezwa nchini Gabon Januari 2017 baada ya kuimenya timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mabao 4-1.

Meneja wa timu ya taifa ya soka ya DRC, Florent Ibenge.
Meneja wa timu ya taifa ya soka ya DRC, Florent Ibenge. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Mabao ya DRC yamewekwa kimyani na Neeskens Kebano katika dakika ya 28, Firmin Mubele Ndombe katika dakika ya 45, Bolingi Mpangi katika dakika ya 72 na Jordan Botaka katika dakika ya 90 ya mchezo. Hata hivyo matokeo hayo yamepunguzwa na Enza, mchezaji wa Jamhuri ya Afrika ya Kati katika dakika ya 62. Vijana wa Florent Ibenge wamemaliza wakiwa kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na alama 15 katika Kundi B mbele ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo imemaliza ikiwa na alama 10 pointi.

Hakutakuwa na wakati viewing kati ya wapinzani wawili. Leopards timidly kuanza mchezo, wakati Waafrika Kati kuweka mguu juu ya accelerator mwanzoni mwa mkutano.

DRC Iliongoza kwa bao moja kwa nunge katika dakika 45 za kwanza. Bao la kwanza la DRC liliwekwa kimyani katika dakika ya 28 na mchezaji Neeskens Kebano,kupitia pasi safi ya Yannick Bolasie. Kwa sasa, DRC ina alama 15 na imefuzu moja kwa moja katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayochezwa ncini Gabon Januari 2017. Hii itakuwa nii kwa mara ya18 timu ya taifa ya soka ya DRC kushiriki katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.