Pata taarifa kuu
US OPEN 2016

Radwanska, Serena na Murray watinga hatua ya tatu US Open

Mchezaji tenesi nambari 4 kwa ubora wa mchezo huo upande wa wanawake, Agnieszka Radwanska, alilazimika kupambana na kurejea kwenye mchezo baada ya ku save mara nne kupata alama na kufanikiwa kumfunga Muingereza Naomi Broady anayeshika nafasi ya tatu kwa nchi ya Uingereza na kutinga katika hatua ya pili ya michuano ya US Open.

Andy Murray, mcheza tenesi raia wa Scotland.
Andy Murray, mcheza tenesi raia wa Scotland. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Radwanska alilazimika kupambana na kurejea kwenye mchezo aliokuwa akionekana akipoteza na iushinda kwa mtindo wa aina yake, na kumfunga Broady kwa seti 7-6 (11-9) na 6-3.

Broady ambaye anaorodheshwa katika nafasi ya 82 kwa ubora wa mchezo huo kidunia, alikuwa akicheza mchezo wake wa mzunguko wa pili wa taji la Grand Slam, huku akicheza na mmoja kati ya wachezaji watano mahiri kwa mchezo huo, ikiwa ni mara ya pili katika historia ya uchezaji wake.

Serena Williams akiwa anatoka uwanjani ameinamisha kichwa baada ya kupoteza mchezo wake kwenye michezo ya Rio, 9 Agosti, 2016
Serena Williams akiwa anatoka uwanjani ameinamisha kichwa baada ya kupoteza mchezo wake kwenye michezo ya Rio, 9 Agosti, 2016 REUTERS/Kevin Lamarque

Kwenye mchezo mwingine, mchezaji nambari moja kwa ubora wa mchezo huo dunianim Serena Williams alimfunga Mmarekani mwenzake Vania King kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-3 na 6-3.

Kwa upande wa wanaume mchezaji Andy Murray na Dan Evans waliungana na Kyle Edmund kuingia hatua ya tatu ya michuano ya US Open, ikiwa ni mara ya kwanza kwa waingereza watatu kutinga kwa pamoja kwenye hatua hiyo toka mwaka 1968.

Murray alishinda kwa seti tatu bila kwa matokeo ya 6-4, 6-1 na 6-4 kwenye uwanja wa Arthur Ashe jijini New York.

Evans yeye alimfunga Mjerumani Alexander Zverev kwa matokeo ya seti 6-4, 6-4, 5-7 na 6-1 kutinga hatua ya 3 ya michuano hiyo katika kipindi cha miaka mitatu.

Murray sasa atacheza na Muitaliano Paolo Lorenzi wakati Evans atacheza na Mswiss, Stan Wawrinka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.