Pata taarifa kuu
USAJILI-MANUTD

Man U yakamilisha usajili wa Paul Pogba, yaweka rekodi

Klabu ya Manchester United hatimaye imefanikiwa kumsajili aliyewahi kuwa mchezaji wake wakati fulani, Paul Pogba, kutoka klabu ya Juventus ya nchini Italia, kwa dau lililoweka rekodi ya dunia.

Mchezaji wa Ufaransa, Paul Pogba akijaribu kumiliki mpira, wakati wa michuano ya kombe la mataifa Ulaya, 2016
Mchezaji wa Ufaransa, Paul Pogba akijaribu kumiliki mpira, wakati wa michuano ya kombe la mataifa Ulaya, 2016 REUTERS/Kai Pfaffenbach Livepic
Matangazo ya kibiashara

Pogba anakuwa mchezaji mwingine ghali zaidi kuwahi kusajiliwa, baada ya usajili wa Chrostian Ronaldo, aliyesajiliwa kutoka klabu ya Manchester United kwenda Real Madrid ya Uhispania kwa dau la pauni milioni 85, huku Gareth Bale akisajiliwa kutoka Tottenham kwenda Real Madrid kwa dau la pauni milioni 94.

Manchester United inaweka rekodi ya kutoa kitita kikubwa zaidi cha fedha kukamilisha usajili wa Pogba kutoka klabu ya Juventus, ambapo imemsajili kwa dau la pauni milioni 105, na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani.

Pogba alisajiliwa na vibibi vizee vya Turini, mwaka 2012 akiwa huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake, ambapo akiwa na Juventus alicheza michezo 128 na kufanikiwa kupachika mabao 28.

Paul Pogba akipiga makofi kabla ya mechi hivi karibuni
Paul Pogba akipiga makofi kabla ya mechi hivi karibuni Reuters

Akizungumza kwa mara ya kwanza na televisheni ya Manchester United TV, Pogba amesema, amefurahi kurudi tena kwenye klabu yake ya zamani, na kwamba anaona ni kama amerudi nyumbani.

Pogba amesema amerejea kuja kukamilisha kile ambacho alishindwa kukikamilisha mwaka 2012 wakati anaondoka, na kwamba ni matarajio yake kuona anapata mafanikio akiwa na moja ya klabu kubwa barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.