Pata taarifa kuu

Bolt; Nataka kuweka historia Brazil, akosoa wanaotumia dawa

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt amewatetea wanariadha wenzake wanaoshiriki michezo ya Olimpiki ya jijini Rio, Brazil, akisema hatua zinazochukuliwa zitawaondoa wasio wasafi.

Mwanariadha wa Jamiaca, Usain Bolt akiwa amekaa mkao wa kupigwa picha mara baada ya kumaliza mbio za mita 200 hivi karibuni.
Mwanariadha wa Jamiaca, Usain Bolt akiwa amekaa mkao wa kupigwa picha mara baada ya kumaliza mbio za mita 200 hivi karibuni. Reuters/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa tamasha maalumu, Bolt ambaye ni bingwa mara sita wa michezo ya Olimpiki, alizungumzia kwa hisia suala la matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni.

Michezo ya mwaka huu ilikumbwa na kashfa kubwa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli mchezo, iliyokuwa inawakabili wanamichezo wa Urusi, huku ikikumbukwa pia wanariadha kadhaa walishawahi kuhudumu adhabu za kufungiwa kushiriki michezo ya Olimpiki kama vile mfukuza upepo wa Marekani Justin Gatlin na LaShawn Merritt.

"Watu wanapaswa kuwa na imani," alisema Bolt. "Tunawaondoa wale wasio waaminifu, tunaenda kwenye muelekeo sahihihi."

Lakini mwanariadha huyo akaongeza kuwa "hakuna hakikisho" wakati alipoulizwa ikiwa wanariadha kama hao waruhusiwe kushiriki kwenye mbio zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi na ikiwa kama wako huru na matumizi ya dawa zinazokatazwa mchezoni.

Bolt ambaye awali alisema atastaafu kukimbia baada ya michuano ya dunia ya mwaka 2017, amethibitisha kuwa michezo ya mwaka huu huenda ikawa ni michuano yake ya mwisho kushiriki.

Bolt anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 100 na 200, amesema kuwa analenga kuwa mtu wa kwanza duniani kukimbia chini ya muda wa sekunde 19 katika mbio za mita 200.

Mwanariadha huyu anaweza kuondoka mjini Rio akiwa na taji la tatu mfululizo la michezo ya Olimpiki baada ya kushinda mita 100, 200 na 400x100 katika michezo ya mwaka 2008 na 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.