Pata taarifa kuu
SOKA

Blatter asema adhabu aliyopewa inamtesa sana kiafya

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter amekiri kuwa hatua ya kupigwa marufuku ya kutoshiriki katika maswala ya soka kwa muda wa miaka sita, kumemwathiri kiafya.

Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter
Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na kituo cha Ujerumani cha ZDF, Blatter mwenye umri wa miaka 80 amesema hatua hiyo imemwathiri sana kwa sababu hakutenda kosa lolote.

“Hatua hii iliyochukuliwa dhidi yangu ilinishangaza sana, naendelea kuteseka hadi leo,” amesema.

Mwezi uliopita, Blatter alikwenda kupata matibabu kutokana na saratani ya ngozi ambayo imekuwa ikimsumbua kwa muda mrefu sasa.

Blatter alishtumiwa kwa tuhma za ufisadi baada ya kutoa malipo ya Euro Milioni 1.8 kwa aliyekuwa mmoja wa Makamu wake Michel Platini kati ya mwaka 1999 na 2002.

“Mimi sio mfisadi!” amesisitiza Blatter.

Majaji wa FIFA walikuwa wamempa adhabu ya kutoshiriki katika maswala ya soka kwa muda wa miezi 8, lakini ikapunguzwa kwa muda wa miaka 6 baada ya kukata rufaa.

Blatter aliongoza FIFA kati ya mwaka 1998 hadi 2015.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.