Pata taarifa kuu
CONTE-CHELSEA

Conte azungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza

Kocha mpya wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza, Antonio Conte, amezungumza kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Stamford Bridge.

Kocha mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, akizungumza kwa mara ya kwanza mbele ya waandishi wa habari, Julai 14, 2016
Kocha mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, akizungumza kwa mara ya kwanza mbele ya waandishi wa habari, Julai 14, 2016 Reuters / Andrew Couldridge Livepic
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mkutano wake na wanahabari, Conte, aliwaomba radhi kwakuwa bado hajajifunza vema lugha ya kiingereza, ambapo mara kwa mara aliwaambia waandishi wa habari warudi swali walilouliza.

Kivutio kikubwa kwa Conte, kilikuwa ni namna ambavyo alimudu kujibu maswali ya waandishi wa habari, waliotaka kujua mbinu ambazo atatumia kuhakikisha Chelsea inarejea kwenye ushindani wa ligi kuu ya Uingereza.

Kocha mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, akitambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari, kwa mara ya kwanza, Julai 14, 2016
Kocha mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, akitambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari, kwa mara ya kwanza, Julai 14, 2016 Reuters / Andrew Couldridge Livepic

Akizungumzia wachezaji atakaowasajili na wale aliwawasajili, Conte, amesema kuwa, "kila mchezaji anayesajiliwa na klabu hii, nafikir anajua jukumu lake, na natarajia kuona akitoa mchango kwa timu kuhakikisha inapata matokeo," alisema Conte.

Akuzungumzia kuhusu ni kwanini aliamua kuacha kuifundisha timu ya taifa, Conte, amesema hakuwa na ugomvi wowote na viongozi wa shirikisho la Italia, lakini aliona kuna vitu anakosa kwenye timu ya taifa na ataweza kuvipata akiwa na klabu.

Conte amesema anatarajia kuwa na msimu mzuri ujao, na kuongeza kuwa asingependa kujipa jina lolote wakati huu kama mtangulizi wake Jose Mourinho, lakini akawapa kazi waandishi wa habari kumtafutia jina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.