Pata taarifa kuu
EURO 2016

Kocha Roy Hodgson abwaga manyanga

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson, ametangaza kujiuzulu nafasi yake, kufuatia kipigo ilichopata timu yake dhidi ya Iceland, cha mabao 2-1, katika mchezo wa hatua ya 16 bora siku ya Jumatatu.

Roy Hodgson, aliyekuwa kocha mkuu wa Uingereza kabla ya kujiuzulu Jumatatu jioni.
Roy Hodgson, aliyekuwa kocha mkuu wa Uingereza kabla ya kujiuzulu Jumatatu jioni. Reuters/Carl Recine
Matangazo ya kibiashara

Hodgson mwenye umri wa miaka 68, amekuwa akikinoa kikosi cha Uingereza kwa miaka minne baada ya kuziba nafasi ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Muitaliano, Fabio Capello, lakini ameshinda michezo mitatu kati ya 11 katika mashindano ya kimataifa.

Nchi ya Iceland yenye idadi ya watu laki 3 na elfu 30 pekee, ilikuwa miongoni mwa timu zilizoorodheswa kuwa na kiwango cha chini zaidi cha soka nchini Ufaransa, ikishika nafasi ya 34 kidunia.

"Naomba radhi kwa kuwa itabidi tamatai yake iwe hivi, lakini hivi vitu hutokea." alisema Hodgson.

"Ninamatumaini makubwa kwamba nitaweza kuiona Uingereza tena ikishiriki kwenye michuano ya kimataifa hivi karibuni." aliongeza Hodgson.

Hodgson ambaye ameshinda michezo 33 kati ya 56 aliyoingoza timu hiyo, alikuwa amalize mkataba wake mwisho wa mashindano ya mwaka huu ya kombe la mataifa Ulaya na alikuwa ameanza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya.

Katika mechi nyingine timu ya taifa ya Italia ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Uhispania kwa mabao 2-0 katika mchezo ambao ni wazi Italia ndio walioonekana kuwa na mipango zaidi kuliko Uhispania ambayo ilicheza chini ya kiwango.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.