Pata taarifa kuu
MPIRA WA KIKAPU-RIO OLIMPIKI

LeBron ajitoa timu ya Marekani itakayoenda Rio

Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu nchini Marekani ya Cleveland Cavaliers, LeBron James, ametangaza kujiondoa kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya nchi hiyo, itakayochaguliwa kushiriki michezo wa Olimpiki, jijini Rio, Brazil. 

Mshambuliaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James.
Mshambuliaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James. David Richard-USA TODAY Sports
Matangazo ya kibiashara

LeBron mwenye umri wa miaka 31, ambaye pia ameshinda medali za dhahabu kwenye mechi mbili zilizopita za timu yake, hatosafiri na timu yake ya taifa ya mpira wa kikapu kwenda nchini Brazil.

Mshindi huyu mara nne wa tuzo ya mchezaji mwenye thamani zaidi, MVP, aliiongoza timu yake ya Cavaliers kushinda taji la NBA kwenye fainali dhidi ya Warriors, amesema usiku wa kuamkia leo kuwa "anataka kupumzika."

Kikosi cha timu ya taifa ya Marekani tayari kinawakosa wachezaji muhimu kama, Steph Curry kinara wa timu ya Golden State Warriors, sambamba na James Harden na Chris Paul.

LeBron ni mchezaji pekee wa timu ya taifa ya kikapu ya Marekani, anayeoongoza kwa kufunga alama nyingi, ambapo ana alama 273, na anashika nafasi ya pili kwa wachezaji wenye ribaundi 95.

Watu wa karibuj wa mchezajik huyo wanasema kuwa huenda akawa amejiondoa kutokana na hofu ya virusi vya Zika, vinavyoendelea kusabababisha madhara kwa watoto wanaozaliwa nchini Brazil.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.