Pata taarifa kuu
EURO 2016

Uingereza, Wales, Slovakia na Urusi kwenye mtihani mgumu

Mechi za kundi B za michuano ya kombe la Ulaya 2016, zinatarajiwa kupigwa tena usiku wa leo, ili kujua nani ataibuka kuwa kinara wa kundi hilo kutinga kwenye hatuja ya 16 bora.

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney akiwa na kocha wake, Roy Hodgson.
Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney akiwa na kocha wake, Roy Hodgson. REUTERS/UEFA
Matangazo ya kibiashara

Uingereza yenyewe itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Slovakia, kwenye mchezo ambao ni muhimu kwa timu zote mbili kuhakikisha kila mmoja anachomoza na ushindi.

Uingereza yenyewe inaongoza kundi B kwa sasa ikiwa na alama 4, ikifuatiwa na Wales yenye alama 3, Slovakia alama 3 na Urusi ambayo inashika mkia kwenye kundi hilo ina alama 1.

Mechi ya leo ni muhimu kwa Uingereza kushinda ili kuwaondoa hofu wakosoaji wa timu hiyo pamoja na mashabiki wake ambao tayari waeonesha kutokuwa na imani na kocha mkuu wa timu hiyo, Roy Hodgoson, ambaye licha ya kuwa timu yake inaongoza kundi, bado haijaonesha kiwango kizuri.

Ikiwa Uingereza itapoteza mchezo wa leo, itakuwa imejiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu, na hii hasa inategemea matokeo ya kati ya timu ya taifa ya Wales na Urusi.

Slovakia yenye alama 3 kwenye kundi lake, nayo inahitaji ushindi wa udi na uvumba ili iweze kufuzu kwenye hatua ya 16 bora, kwakuwa ikiwa itashinda mechi yake dhidi ya Uingereza, itafikia alama 6 ambazo zitaweza kuifanya iongoze kundi hilo kutokana na matokeo ya Wales na Urusi yatakavyokuwa.

Roy Hodgson leads his England side into a must win fixture against Wales.
Roy Hodgson leads his England side into a must win fixture against Wales. Reuters/Carl Recine

Kocha wa Uingereza, Roy Hodgson, anasema kuwa, mchezo wa leo utakuwa mgumu kwa timu yake, hasa ukizingatia umuhimu wenyewe wa mchezo wa timu zote mbili, lakini akajipa moyo kuwa hakuna sababu ya timu yake kupoteza mchezo wa leo.

Uingereza yenyewe inahitaji alama moja tu kujihakikishia nafasi ya kuingia kwenye hatuja ya 16 bora ya michuano ya mwaka huu.

Katika mechi nyingine, Wales wenye alama 3, watakuwa na kibarua kigumu wakati itakaposhuka dimbani kuikabili timu ya taifa ya Urusi, ambayo yenyewe ikiwa inataka kubaki kwenye michuano ya mwaka huu ni lazima iibuke na ushindi wa zaidi ya mabao mawili dhidi ya Wales kuwawezesha kufikisha alama 4.

Beki tegemeo wa timu ya taifa ya Croatia, Martin Skrtel, akiwa mazoezini.
Beki tegemeo wa timu ya taifa ya Croatia, Martin Skrtel, akiwa mazoezini. REUTERS/Jason Cairnduff

Kocha wa Urusi, Leonid Slutski, amekiri kuhusu ugumu wa mchezo wa leo, na kuongeza kuwa hata kama timu yake inawachezaji wazuri wenye uzoefu na waliocheza mechi kama hizi, haitoshi kuwapa kiburi kwamba wataibuka na ushindi kwenye mechi ya leo, ila amejipanga kuhakikisha timu yake inaibuka na ushindi.

Kwa upande wake kocha mkuu wa Wales, Chris Coleman, amesema kuwa anafahamu Urusi itakuja kwenye mchezo huo kwa kupania kupata ushindi, lakini na wao ni lazima wajipange kuhakikisha kuwa wanachomoza na ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri zaidi ikiwa wataingia kwenye hatua ya 16 bora.

Wachambuzi wa masuala ya soka wanakosoa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinachonolewa na kocha Roy Hodgson, ambaye wanasema kuwa na wachezaji wengi vijana kwenye timu, ndiko kumeigharimu timu hiyo kutokuwa na makali kwenye michuano ya mwaka huu.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Urusi, wakijishika mdogo baada ya mechi.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Urusi, wakijishika mdogo baada ya mechi. REUTERS/Christian Hartmann Livepic

Hata hivyo Hodgson mwenyewe anasisitiza kuwa kikosi chake kiko kwenye mabadiliko makubwa ya kusukwa na kwamba baada ya miaka michache ijayo, Uingereza itakuwa na kikosi imara ambacho kinawachezaji vijana wanaoweza kutoa ushindani mkubwa kwenye michuani ya kimataifa.

Uingereza leo huenda leo huenda ikwakosa wachezaji wake muhimu kama nahodha, Wayne Rooney ambaye kwa maelezo ya kocha anataka kumpumzisha.

Wales yenyewe itaingia uwanjani ikimtegemea mshambuliaji wake wa kimataifa anayekipiga na timu ya Real Madrid ya Uhispania, Gareth Bale ambaye amekuwa chachu kubwa kwa timu yake kuanza vema michuani ya mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.