Pata taarifa kuu
EURO 2016

Griezmann, Payet waipeleka Ufaransa 16 bora, leo ni Wales na Uingereza

Magoli yaliyofungwa kwenye dakika za lala salama na wachezaji, Antoine Griezmann na Dimitri Payet, yalitosha kuipa tiketi ya kifuzu kwenye hatua ya 16 bora Ufaransa, baada ya kukumbana na upinzani mkali toka kwa timu ya taifa ya Albania. 

Mchezaji Olivier Giroud, akiruka juu kujaribu kuifungia timu yake goli la kuongoza
Mchezaji Olivier Giroud, akiruka juu kujaribu kuifungia timu yake goli la kuongoza REUTERS/Eddie Keogh Livepic
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid ya Uhispania, Griezmann akitokea benchi, aliipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 90 ya mchezo kabla ya mchezaji wa West Ham United, Dmitri Payet kupigilia msumari wa mwisho sekunde chache kabla ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha kumaliza mpira dakika ya 95.

Payet pia ndiye aliyekuwa kinara wa timu yake kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya mwaka huu, baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza na la ushindi, wakati Ufaransa ilipocheza na Romania na kushinda kwa mabao 2-1.

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, amewaambia waandishi wa habari baada ya mchezo wao dhidi ya Albania, kuwa aina hii ya ufungaji imeshakuwa kama tabia kwa timu yao lakini angetamani mara zote awe anapata mabao ya dakika za mwanzo kabisa.

Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia moja ya goli lililofingwa na timu yao dhidi ya Albania.
Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia moja ya goli lililofingwa na timu yao dhidi ya Albania. 路透社

Ushindi huu wa Ufaransa ambao unawavusha kuingia kwenye hatua ya 16 bora, tayari umeleta matumaini kuwa huenda timu hiyo ikarudia historia ya mwaka 1984 kwenye michuano ya Ulaya na mwaka 1998 wakati wa fainali za kombe la dunia, ambapo ilifanikiwa kuchukua mataji hayo kwenye ardhi yake ya nyumbani.

Deschamps katika hatua ya kushangaza, aliwaacha nje mchezaji wa Juventus, Paul Pogba na Antione Griezmann, wachezaji ambao walikuwa mwiba kwenye mchezo wao wa awali dhidi ya Romania.

Kwenye mechi nyingine zilizochezwa hapo haja, Urusi iliangukia pua baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Slovakia, huku Romania wakilazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya taifa ya Uswis.

Leo kutakuwa na michezo mitatu itakayopigwa, ambapo saa kumi kamili kwa saa za hapa Afrika Mashariki, Uingereza itacheza na majirani zao Wales, huku Ukraine wakiwa wenyeji wa Ireland ya Kaskazini na Ujerumani ikiwa mwenyeji wa timu ya taifa ya Poland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.