Pata taarifa kuu
EURO 2016

Ujerumani kuanza safari ya kutafuta ubingwa wa bara Ulaya

Michuano ya soka kuwania taji la bara Ulaya yameingia siku ya tatu leo Jumapili nchini Ufaransa.Leo ni zamu ya kundi C na D.

Uwanja wa soka wa Pierre Mauroy mjini Lille
Uwanja wa soka wa Pierre Mauroy mjini Lille UEFA Photos
Matangazo ya kibiashara

Mchuano wa kwanza ni wa kundi D kati ya Uturuki na Croatia kuanzia saa 10 Kamili saa za Afrika Mashariki.

Uturuki ikipambana na Croatia
Uturuki ikipambana na Croatia UEFA Photos

Mambo muhimu kuhusu timu hizi mbili:
Zimekutana mara sita kabla ya mchuano huu wa leo.

Croatia imeshinda mara mbili, na michuano minne timu nne zimetoka sare, ikiwa ni pamoja na michuano ya bara Ulaya ya mwaka 2008, hatua ya robo fainali mechi ambayo baadae Uturuki ilishinda kwa mikwaju ya penalti.

Uturuki, imepoteza mechi zao zote tatu katika michuano mitatu ya ufunguzi ya kutafuta ubingwa wa taji hili.

Croatia imepoteza tu mchuano mmoja wa makundi katika michuano sita iliyopita ya michuano hii katika hatua ya makundi.

Poland vs Ireland Kaskazini

Timu ya taifa ya Poland wakifanya mazoezi
Timu ya taifa ya Poland wakifanya mazoezi UEFA Photos

Mechi hii inaanza saa Moja Kamili jioni saa Afrika Mashariki.

Mambo muhimu kuhusu timu hizi mbili:-
Katika mechi mbili ambazo timu zimekutana, Ireland Kaskazini haijafungwa. Imeshinda mechi moja na kutoka sare nyingine.

Mara ya mwisho kukutana katika michuano ya Ulaya ilikiwa ni mwaka 1962, na Ireland Kaskazini na kushinda kwa mabao 2 kwa 0.

Hii ni mara ya tatu kwa Poland kushiriki katika michuiano hii.

Poland haijawahi kushinda mechi yoypte katika michuano hii ya bara Ulaya, imetoka sare mara 3 na kupoteza mechi 3.

Ujerumani vs Ukraine

Mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil
Mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil UEFA Photos

Mechi inaanza saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.

Ukraine haijawahi kuishinda Ujerumani katika michuanio mitano iliyopita.
Hii ndio mara ya kwanza kwa timu hizi mbili kukutana katika michuano hii ya bara Ulaya.

Ujerumani inashiriki katika michuano hii mara 12 na imeshinda mara tatu mwaka 1972, 1980 na 1996.

Mwaka 1984, 2000 na 2004 ilifikia hatua ya makundi ya michuano hii.

Ujerumani haijawahi kupoteza mechi ya ufunguzi katika michuano hii ya bara Ulaya.

Ukraine iliondolewa katika hatua ya makundi iliposhiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.