Pata taarifa kuu
AFRIKA

Nigeria yapata pigo jingine kwenye soka

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Shuaibu Amodu amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58, shirikisho la mpira nchini Nigeria, NFF, limetangaza kwenye tovuti yake.

Shuaibu Amodu kocha wa zamani wa Nigeri
Shuaibu Amodu kocha wa zamani wa Nigeri NFF
Matangazo ya kibiashara

Amodu alikuwa mkurugenzi wa ufundi wa NFF, ambapo aliwahi pia kuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa, Super Eagles kwa zaidi ya mara nne, na alikuwa akilalamika kupata maumivu ya kifua.

Amodu aliiongoza Nigeria kwenye mechi za kufuzu mwaka 2002 na 2010 wakati wa kombe la dunia, lakini akajikuta akifutwa kazi hata kabla ya michuano yenyewe.

Kifo cha Amodu kimekuja ikiwa ni siku tatu tu zimepita toka kufariki kwa aliyewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi "Big Boss" aliyefariki akiwa na umri wa miaka 54.

Rais wa shirikisho la NFF, Amaju Pinnick, amesema "hili ni tukio jingine baya. Bado tunazungumza kuhusu kifo cha Keshi na sasa Amodu nae hayupo. Kwakeli sina maneno ya kueleza."

Amodu alikuwa achukue nafasi ya Sunday Oliseh, ambaye alijiuzulu kukifundisha kikosi cha Nigeria mwezi February lakini akakataa kuchukua jukumu hilo kwa sababu za kiafya.

Amodu amewahi kuzifundisha timu za Afrika Kusini, kama vile Orlando Pirates kati ya mwaka 1996 na 1997.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.