Pata taarifa kuu
EURO 2016 - UFARANSA

Uefa kumruhusu Platin kutazama mechi zote

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya, aliyefungiwa na Fifa kujihusisha na masuala ya soka, Michel Platin, ataruhusiwa kuhudhuria mechi za kombe la mataifa ya Ulaya lakini ametakiwa kutojihusisha kwa namna yoyote na masuala ya kiofisi. 

Michel Platini, rais wa zamani wa shirikisho la mpira Ulaya, sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka 6 kujihusisha na soka
Michel Platini, rais wa zamani wa shirikisho la mpira Ulaya, sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka 6 kujihusisha na soka Reuters/Eric Gaillard/Files
Matangazo ya kibiashara

Kaimu katibu mkuu wa shirikisho la mpira Ulaya, amesema kuwa ofisi yake imepokea taarifa kutoka shirikisho la mpira la dunia Fifa, likiwaeleza kuwa Michel ataruhusiwa kushuhudia mechi za Euro kama shabiki mwingine yeyote, isipokuwa tu hataruhusiwa kujihusisha na masuala ya utawala, amesema Theodore Theodoridis.

Katibu mkuu huyo ameongeza kuwa, baada ya kupokea taarifa hiyo, kamati ya utendaji ya UEFA itaketi kuamua ikiwa itamualika rais huyo wa zamani wa shirikisho la mpira Ulaya kushuhudia mechi zote.

Reuters

UEAF inasema kuwa Michel Platini hatarajiwi kuhudhuria mechi ya ufunguzi itakayofanyika Ijumaa ya wiki hii ambapo wenyeji Ufaransa watakuwa wanafungua pazia dhidi ya Romania.

Hata hivyo katibu mkuu wa UEFA amesema kuwa licha ya kutarajiwa kwa uamuzi wa kamati ya utendaj kuhusu Platin, kiongozi huyo bado hajathibitisha ikiwa angetaka kuhudhuria mechi yoyote.

Shirikisho hilo linatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu mwezi September mwaka huu kuchagua mrithi wa Platin, hii ikimaanisha kuwa UEFA itakuwa haina rais wakati wote wa michuano ya Ulaya inayoanza Juni 10 hadi Julai 11 nchini Ufaransa.

Platin, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi kuwa na mafanikio makubwa wakayi akiichezea timu hiyo, lakini akajikuta matatani baada ya kukubali malipo tata kutoka kwa aliyekuwa rais wa Fifa, Sepp Blatter.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.