Pata taarifa kuu
FIFA-BENIN

FIFA yaichukulia vikwazo Benin

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limeifungia Benin kushiriki katika maswala yote ya soka duniani kwa muda usiojulikana.

Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015.
Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

FIFA imechukua hatua hiyo baada ya Mahakama nchini Benin mapema mwezi huu kutoa uamuzi wa kusimamisha uchaguzi uliokuwa umepangwa hivi karibuni kuwachagua viongozi wa Shirikisho la soka nchini humo.

Uamuzi huu unamaanisha kuwa Benin watakosa mchuano muhimu kufuzu kucheza fainali ya mataifa ya Afrika dhidi ya Equitorial Guinea mwezi ujao.

Kanuni za FIFA haziruhusu serikali kuingilia kati usimamizi wa soka hata kama kuna mzozo wa viongozi wa soka.

Uamuzi huu umeamuliwa wakati wa kuanza kwa mkutano Mkuu wa FIFA nchini Mexico.

Pamoja na hilo, Baraza la FIFA limeidhinisha rasmi Kamati maalum kusimamia maswala ya soka nchini Guinea kutokana na mzozo wa viongozi wa Shirikisho la soka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.