Pata taarifa kuu
SOKA-TANZANIA

Yanga FC na Azam FC Kumenyana mwishoni mwa juma

Yanga FC na Azam FC zitachuana katika fainali ya kuwania taji la Shirikisho nchini Tanzania baada ya ushindi katika michuano ya nusu fainali mwishoni mwa juma lililopita.

Uwanja wa Taifa wa soka jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Uwanja wa Taifa wa soka jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Matangazo ya kibiashara

Mchuano wa Yanga dhidi ya Coastal Union ugenini katika uwanja wa Mkwakani mjini Tanga, ulisitishwa katika muda wa ziada baada ya mashabiki wa nyumbani kuzua fujo.

Mmoja wa marefarii wasaidizi alijeruhiwa baada ya kupigwa mawe na mashabiki wa Coastal Union waliokuwa na hasira baada ya kupinga bao la 2 walilodai lilifungwa kwa mkono na Hamis Tambwe.

Pamoja na vurugu hizio, Yanga walimaliza mchuano huo kwa ushindi wa mabao 2 kwa 1 wakiwa ugenini.

Coastal Union walianza kwa kufunga lakini mambo yakawa mabaya baada ya Yanga kusawazisha na kufunga bao la pili.

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF linasubiriwa kutoa maamuzi kuhusu tukio hilo ambalo limekashifiwa na wadau wa soka kwa mashabiki kuchukua hatua mikononi mwao lakini namna marefarii walivyoucheza mechi hiyo.

Azam FC nayo ikicheza mjini Shinyanga dhidi ya Mwadui FC ilitoka sare ya mabao 2 kwa 2 lakini ikafuzu kwa kupata penalti 5 dhidi ya 2 baada ya kumalizika kwa muda wa ziada wa dakika 30 na ule wa kawaida wa dakika 90.

Fainali hiyo itachezwa mwezi Mei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.