Pata taarifa kuu
FA-CHELSEA-MAN CITY-SOKA

Man City yaburuzwa na Chelsea

Chelsea wakicheza wakichezea nyumbani Stamford Bridge wameweza kuwaburuza Manchester city kwa mabao 5-1, katika michuano ya Kombe la FA inayoendelea. Siku ya Jumapili peke timu tisa zimlijitupa uwanjani katika michezo mitatu.

Wachezaji wa Manchester City na Chelsea wakizozana kwenye moja ya mechi walizokutana, na sasa walikukutana Jumapili hii Februari 21, 2016 katika raundi ya tano michuano ya FA 2016.
Wachezaji wa Manchester City na Chelsea wakizozana kwenye moja ya mechi walizokutana, na sasa walikukutana Jumapili hii Februari 21, 2016 katika raundi ya tano michuano ya FA 2016. YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Chelsea ilifanikiwa kupata ushindi huo kupitia mabao yalioingizwa na wachezaji Diego Costa , Willian borges , Gary Cahill ,Eden Hazard. Bao lawisho ambalo ni la tano lilifungwa na mchezaji Bertrand Traore katika dakika ya 89 ya mchezo.

Bao la kufuta machozi la Manchester city lilifungwa na mchezaji David Faupala.

Wakati huo huo Blackburn Rovers iliangukia pua kwa kufungwa na West Ham mabao 5-1, nao Crystal Palace wakiwafunga Tottenham mbao 1-0.

Chelsea kwa sasa inajiandaa kutimua vumbi na Everton katika mchezo wa Robo Fainali baada ya kuiondoa Manchester City. Crystal Palace watamenyana na Reading, katika uwanja wa Watford.

Shrewsbury Town au Manchester United wataipokea West Ham United.

Hull City watarudiana na Arsenal kuwania hatua ya Robo Fainali, baada ya kutoka sare ya kutofunganakatika mchezo wa Jumapili hii katika uwanja wa Emirates, wakati ambapo Shrewsbury Town wataikaribisha Manchester United Jumanne wiki hii katika uwanja wa New Meadow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.